Skip to main content

Usaidizi wa Gemini unaokufaa

Pata usaidizi wa AI inayokuelewa.

Usaidizi unaokufaa

Kwa kutumia Gemini, tunatayarisha kiratibu binafsi kinachotumia AI. Kiratibu ambacho kando na kujibu maswali ya jumla kinakuelewa — kwa kutoa usaidizi kulingana na ari, udadisi na mambo yanayokuvutia. Ina manufaa yafuatayo:

Angalia usaidizi zaidi unaoweza kupata kulingana na Historia ya mambo uliyotafuta

Boresha wazo linalofuata

Pata mawazo maalum yanayoendana na ari pamoja na malengo yako ya kipekee, yanayokusaidia kuanzisha mradi wako ujao.

    Gemini prompt that reads "I want to start a YouTube channel, but need some content ideas."

    Gundua chaguo zinazokufaa

    Angalia mapendekezo uliyochaguliwa kulingana na mapendeleo yako, hivyo kuokoa muda wako na kukuletea mambo ambayo bila shaka utayapenda.

      Gemini prompt that reads "What's a hidden gem I haven't discovered yet in San Diego?"

      Gundua udadisi wako

      Gundua mtazamo wa kipekee uliowekewa mapendeleo kulingana na shughuli zako mtandaoni.

        Gemini prompt that reads "What's a new hobby I should try?"

        Unadhibiti faragha yako

        Tumejitolea kuhakikisha kuwa kuna uwazi na kukupatia udhibiti.

        Unachagua cha kutuma

        Si lazima utumie vipengele vya Gemini vya kuweka mapendeleo. Unaamua iwapo ungependa kuunganisha Historia ya mambo uliyotafuta, kutuma mapendeleo binafsi au kuwasha historia ya gumzo.

        Dhibiti data yako kwa urahisi

        Fikia mipangilio yako ya Gemini ili uangalie na udhibiti taarifa ulizohifadhi na magumzo ya awali. Unaweza pia kuangalia na kudhibiti Historia ya mambo uliyotafuta kupitia Shughuli kwenye Programu na Wavuti.

        Uwazi wa kuaminika

        Mfumo wetu wa uchanganuzi wa kina unatoa muhtasari kamili wa jinsi Gemini inavyowekea majibu mapendeleo na inaweza kukuonyesha vyanzo vya data — taarifa ulizohifadhi, magumzo ya awali au Historia ya mambo uliyotafuta — iliyotumiwa.

        Usaidizi unaokufaa umerahisishwa

        Pata taarifa sahihi, kwa wakati unaofaa, kwa njia sahihi. Gemini iliyo na uwezo wa AI wa kuweka mapendeleo hukurahisishia maisha, kwa kutoa pendekezo linalokufaa, moja baada ya nyingine.

        Maswali yanayoulizwa sana

        Uwezo wa kuweka mapendeleo, unaoendeshwa na mfumo wa Gemini wa majaribio wa 2.0 Flash Thinking, ni uwezo wa majaribio unaoiwezesha Gemini kutumia Historia ya mambo uliyotafuta ili kukupatia majibu yanayokufaa.

        Unafanya kazi kwa kuchanganua kidokezo chako na kubaini iwapo Historia ya mambo uliyotafuta hapo awali inaweza kusaidia katika kutayarisha jibu. Unafanya hivi kwa kuhakikisha kuwa maelezo unayopokea yametayarishwa kulingana na mahitaji na mambo yanayokuvutia.

        Uwezo huu unapatikana kwenye Gemini 2.0 Flash Thinking ukiwa ni jaribio.

        Gemini iliyo na uwezo wa kuweka mapendeleo inazinduliwa ikiwa kipengele cha majaribio, kinachopatikana kwa waliojisajili kwenye Gemini Advanced na Gemini katika wavuti leo na kinasambazwa kwa utaratibu kwenye simu. Hali hii bado haipatikani kwa watumiaji wa Google Workspace au Google Workspace for Education walio na umri wa chini ya miaka 18. Vikomo vya matumizi vya siku zijazo vinaweza kutumika.

        Inapatikana katika zaidi ya lugha 45 na katika nchi nyingi duniani kote, isipokuwa nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya, Uswizi na Uingereza.