Pata usaidizi wa kutekeleza majukumu katika programu mbalimbali kwa wakati mmoja
Ukitumia programu, sasa unaweza kupata mihtasari kutoka kwenye Gmail yako, kuweka bidhaa kwenye orodha yako ya vyakula kwa urahisi katika Google Keep, kupanga vidokezo vya usafiri vya rafiki yako papo hapo kwenye Ramani za Google, kutayarisha orodha maalum kwenye YouTube Music na mengine mengi.
Pata maelezo sahihi katika barua pepe zako
Iombe Gemini iandae muhtasari wa barua pepe kutoka kwa anwani fulani au itafute maelezo mahususi kwenye kikasha chako.
Furahia muziki mpya
Cheza, tafuta na ugundue nyimbo, orodha pamoja na wasanii unaowapenda. Iombe Gemini itayarishe orodha inayofaa wakati wowote – kama vile orodha maalum ya nyimbo bora tangu 2020.
Panga siku yako kwa ufanisi
Iruhusu Gemini ipange kalenda yako na ikusaidie kufuatilia matukio. Piga picha ya kipeperushi cha tamasha na uiombe Gemini iandae tukio la kalenda kulingana na maelezo hayo.
Pata maarifa kutoka kwenye vitabu vya kujifunzia vinavyoaminika
Gemini inaweza kupata maelezo kutoka kwenye vitabu vya kujifunzia kwa kutumia OpenStax, mpango wa kielimu usiolenga faida wa Chuo Kikuu cha Rice. Iulize Gemini kuhusu dhana au mada yoyote na upate maelezo mafupi yenye viungo vya kuelekeza kwenye maudhui husika ya vitabu vya kujifunzia.