Gemini Canvas
Fanya mawazo yako yawe uhalisia kama vile programu, michezo, michoro yenye maelezo na mengineyo. Fanya vidokezo vyako viwe mifano ya awali kwa haraka, ukitumia uwezo wa Gemini 2.5 Pro, mfumo wetu wenye uwezo zaidi.
Canvas ni nini
Kupata taswira na Kuwekea mapendeleo
Geuza ripoti zako za Deep Research ziwe programu, michezo, maswali shirikishi, kurasa za wavuti, michoro yenye maelezo, kubadilisha unavyojifunza, kugundua na kutuma maarifa.
Kudokeza na Kutayarisha
Elezea tu wazo lako kisha Canvas itabuni msimbo utakaosanidi programu au mchezo unaofanya kazi, unaoweza kutuma.
Kuandika na Kuboresha
Boresha uandishi wako kwa kuandaa rasimu zinazovutia, kuimarisha toni, kuboresha sehemu muhimu pamoja na kupata maoni yenye maarifa papo hapo.
Pakia mwongozo na vyanzo vya mafunzo, Gemini itatayarisha maswali maalum ili kufanya mafunzo yawe ya kushirikisha zaidi. Yatumie kutathmini uelewa wako au uwatumie marafiki na familia kiungo ili muwe na shindano la kufurahisha.
Imarisha uelewa wako wa dhana fiche kwa kutazama uhuishaji wa jinsi algoriti zinavyotekelezwa na kubadilisha mawazo changamano yawe hoja dhahiri zinazoonyesha jinsi msimbo unavyofanya kazi.
Boresha hati, utafiti au hotuba zako ukitumia Gemini. Zana za kubadilisha kwa haraka hukusaidia kupanua sehemu muhimu, kurekebisha toni na kupata maoni yenye maarifa kuhusu rasimu yako.
Harakisha mchakato wa kutoka uchanganuzi hadi mikakati ukitumia Gemini, ili ikusaidie katika kuchangia mawazo, mapendekezo na kuimarisha bidhaa za ubora wa juu kwa haraka ili kuokoa muda na kupata matokeo.
Boresha utendaji wa timu zako kwa kutumia dashibodi zilizoundwa maalum iwe ni vifuatiliaji vya timu au mifumo ya usimamizi wa wateja na ya hatua za mauzo, hivyo kufanya watu wote wapate taarifa na kurahisisha utaratibu wa kazi.
Harakisha na ubadilishe upendavyo makadirio katika muda halisi ukitumia kitelezi cha bei kinachoshirikisha. Iwezeshe timu yako kutoa mapendekezo yanayofaa papo hapo, ambayo yanakuza mazungumzo na kuongeza ushawishi wa kuchukua vitendo.
Tayarisha ulimwengu wako wa kubuni wa 3D. Bonyeza upau wa nafasi ili ubuni sayari anuai zenye maelezo ya kipekee papo hapo.
Jaribu uwezo wako wa kukumbuka sauti katika shindano la kufurahisha. Bofya kadi, sikiliza sauti kisha utafute sauti zinazolingana.
Tunga muziki kwenye zana ya dijitali ya kusanisi ili kujaribu sauti na kuunda midundo.
Pata taswira ya algoriti zikifanya kazi, kama vile algoriti hii ya Breadth-First Search. Tumia gridi hii kufuata njia ya algoriti kutoka inapoanzia hadi inakoishia na utazame kila kisanduku kilichotembelewa kikiwaka kinapopata njia fupi zaidi hata kukiwa na vizuizi.
Maswali Yanayoulizwa Sana
Kuanza ni rahisi. Chini ya upau wa kidokezo, chagua “Canvas” kisha uweke kidokezo chako ili ufungue hati au uanzishe mradi wa usimbaji.
Canvas inapatikana kwa watumiaji wote wa Gemini. Waliojisajili kwenye Google AI Pro na Google AI Ultra wanaweza kutumia Canvas kwenye mfumo wetu wa Gemini 2.5 Pro ulio na uwezo zaidi pamoja na kiwango kikubwa zaidi cha kubaini muktadha chenye tokeni milioni 1 kwa miradi changamano zaidi.
Chagua Deep Research chini ya upau wa kuandika kidokezo. Ripoti yako ya Deep Research itatayarishwa katika Canvas mpya. Baada ya utafiti kukamilika, utaona kitufe cha “Tayarisha” katika sehemu ya juu kulia ya Canvas. Bofya “Tayarisha,” kisha utaona chaguo za kuunda ukurasa wa wavuti, mchoro wenye maelezo, maswali au muhtasari kwa sauti kwenye menyu kunjuzi. Teua mojawapo ya chaguo hizi kisha Canvas italifanya liwe uhalisia.
Ndiyo, unaweza kufikia miradi yako ya Canvas kwenye programu yako ya simu. Tafadhali kumbuka kuwa unaweza tu kubadilisha mtindo na muundo wa maandishi katika programu ya Gemini ya wavuti kwenye kompyuta ya mezani. Utendaji huu haupatikani kwenye vifaa vya mkononi.
Canvas inapatikana kwa watumiaji wa Gemini katika lugha na nchi zote ambako Programu ya Gemini inapatikana.