Skip to main content

Buni upya picha zako ukitumia kidokezo

Tumia picha zako kufanya mambo mengi zaidi. Chukulia kuwa upo katika mandhari tofauti, unganisha vipengele vya ubunifu, fanya mabadiliko mahususi na mambo mengine mengi. Kitakachokuzuia ni ubunifu wako tu.

Picha zako, maono yako

Tumia ubunifu wako kujiweka popote

Jipeleke katika maeneo na karne mbali mbali, vaa mavazi tofauti au hata ujaribu mitindo tofauti ya nywele.

Weka pamoja picha zako

Unaweza kupakia picha nyingi kwa wakati mmoja ili uweke pamoja na uchanganye vipengele katika mandhari yale yale.

Andaa mseto wa picha zako

Hamisha muundo, rangi au umbile la kitu kimoja kisha uyatumie kwenye kitu kingine.

Fanya mabadiliko mahususi

Badilisha kwa urahisi vipengele mahususi kwenye picha zako kwa kutumia maneno tu. Rejesha picha, badilisha mandharinyuma, badilisha yaliyo kwenye picha na mambo mengine zaidi.

Buni picha kwa haraka

Buni picha za kuvutia kwenye Gemini ukitumia Imagen 4, mfumo wetu bora zaidi wa kubadilisha maandishi kuwa picha. Badilisha kwa urahisi mawazo yako yawe picha zilizo na taswira dhahiri na uhalisia wa kupendeza.

Na kuhusu herufi…

Imagen 4 hutoa maandishi katika kiwango kipya cha usahihi.

Weka vipimo vipya,
kirahisi.

Kwa ubayana zaidi

Buni katika muundo wowote

Gundua ubunifu wa ajabu

Maswali yanayoulizwa sana

Kipengele cha kubuni picha kwa kutumia AI kinapatikana katika lugha zote na nchi zote ambamo programu ya Gemini inapatikana.

  1. Anza na fomula rahisi. Jaribu <Tayarisha/buni picha ya>  <mada> <kitendo> <tukio> kisha uendelee ukianzia hapo. Kwa mfano, "Tayarisha picha ya paka akiwa amelala chini ya mwale wa jua kwenye fremu ya chini ya dirisha."

  2. Toa maelezo mahususi kadri ya ubunifu wako. Vidokezo vinapaswa kuwa na maelezo mengi mahususi kadri ya ubunifu wako, kwa hivyo, badala ya kusema, "Buni picha ya mwanamke aliyevaa nguo nyekundu," jaribu "Buni picha ya mwanamke aliyevaa nguo nyekundu huku akikimbia kwenye bustani." Kadri unavyotoa maelezo ya kina ndivyo Gemini itaweza kufuata maagizo yako.

  3. Zingatia utunzi, muundo na ubora wa picha. Fikiria kuhusu jinsi unavyotaka vipengele vya picha yako vipangwe (utunzi), mwonekano unaoutaka (muundo), kiwango unachotaka cha ubora wa picha (ubora wa picha) na uwiano (ukubwa). Jaribu kitu kama vile, "Buni picha iliyotiwa ukungu ya nungu mwenye miba huku akipaa angani ukitumia mbinu ya upakaji rangi ya mafuta na uwiano wa 2:3."

  4. Ubunifu wako utakusaidia. Gemini ni bora kwa kubuni vitu vya ajabu na matukio ya kipekee. Panua mawazo yako.

  5. Usipopenda untakachoona, iombe Gemini ikibadilishe. Kupitia mfumo wetu wa kubadilisha picha, unaweza kudhibiti picha zako kwa kuiambia Gemini ibadilishe mandharinyuma, ibadilishe kitu kimoja na kingine au iongeze kipengele huku ikihifadhi maelezo unayotaka.

Kulingana na Kanuni zetu za AI, Zana hii ya kubuni picha za AI iliundwa ili iweze kutumika kwa kuwajibika. Ili kuhakikisha kuwa kuna utofautishaji wazi kati ya picha zilizobuniwa na Gemini na kazi halisi ya sanaa ya binadamu, Gemini hutumia SynthID alama maalum isiyoonekana pamoja na alama maalum inayoonekana ili kuonyesha kuwa zimetayarishwa kwa AI.

Matokeo ya Gemini hutegemea kimsingi vidokezo vya mtumiaji na sawa na zana yoyote ya AI zalishi, kunaweza kuwa na matukio ambapo inatayarisha maudhui ambayo baadhi ya watu binafsi wanaweza kuyapinga. Tutaendelea kuzingatia maoni yako kupitia vitufe vya nimeipenda au sijaipenda na tutaendelea kufanya maboresho. Kwa maelezo zaidi, unaweza kusoma kuhusu mbinu tunazotumia kwenye tovuti yetu.