Tayarisha video zenye sauti ukitumia Veo 3
Tayarisha video za sekunde 8 zenye ubora wa juu ukitumia Veo 3, mfumo wetu mpya kabisa wa kutayarisha video unaotumia AI. Jaribu ukitumia mpango wa Google AI Pro au upate kiwango cha juu zaidi ukitumia mpango wa Ultra. Fafanua tu kile unachokiwazia na uone mawazo yako yakigeuzwa kuwa uhalisia kupitia utayarishaji wa sauti unaofanywa na mfumo wenyewe.
Veo 3 Ina manufaa mengi
Liwaze. Lifafanue. Tosha.
Kugundua
Tumia mitindo anuai, huisha wahusika na uunganishe vitu ukitumia njia ambazo hukuwahi kutarajia kuwa zinawezekana. Angalia unachoweza kutayarisha.
Sambaza
Tayarisha meme za kuchekesha, geuza mizaha iwe video, anzisha upya matukio maalum na uweke mapendeleo ili umfanye mtu atabasamu.
Kuchangia Mawazo
Tayarisha maudhui yenye ubunifu zaidi na uonyeshe mawazo yako kwa haraka. Iwe ni dhana na miundo ya bidhaa au uandaaji wa mifano ya awali na usimuliaji wa hadithi kwa haraka, Gemini inaweza kusaidia.
Fahamu zaidi kuhusu Mifumo yetu ya Veo
Kwa kuendeshwa na Veo 3 Fast, Gemini inaweza kugeuza picha na maandishi ya kawaida yawe video nyumbufu zenye sauti maalum.
Tayarisha video za sekunde 8 zenye ubora wa juu zilizo na sauti ukitumia mfumo wetu wa hali ya juu wa kutayarisha video.
Maswali yanayoulizwa sana
Ndiyo, unaweza kutayarisha na kutuma video kwenye programu yako ya Gemini ya vifaa vya mkononi. Ili utayarishe video, gusa kitufe cha "video" katika upau wako wa kuandika vidokezo. Ikiwa hukioni, gusa kitufe chenye vitone vitatu ili uangalie chaguo zaidi.
Jaribu Veo 3 Fast ukitumia mpango wa Google AI Pro au upate kiwango cha juu zaidi cha Veo 3 kwenye Google AI Ultra, inayopatikana katika zaidi ya nchi 70.
Veo 2 inapatikana katika nchi ambapo mifumo ya Veo 3 haipatikani.
Tumechukua hatua kadhaa muhimu za usalama ili kufanya utayarishaji wa video kwa kutumia AI uwe salama. Hii ni pamoja na majaribio ya kina ya kidukuzi na kihasidi ili kulinda shirika na ukaguzi unaolenga kuzuia utayarishaji wa maudhui yanayokiuka sera zetu. Vile vile, video zote zinazotayarishwa kwa kutumia Veo katika programu ya Gemini huwekewa alama maalum inayoonekana na SynthID, alama maalum ya kidijitali inayopachikwa katika kila fremu, inayoonyesha kuwa video zimetayarishwa kwa AI.
Matokeo ya Gemini hutegemea kimsingi vidokezo vya mtumiaji na sawa na zana yoyote ya AI zalishi, kunaweza kuwa na matukio ambapo inatayarisha maudhui ambayo baadhi ya watu binafsi wanaweza kuyapinga. Tutaendelea kuzingatia maoni yako kupitia vitufe vya nimeipenda au sijaipenda na tutaendelea kufanya maboresho. Ili upate maelezo zaidi, unaweza kusoma kuhusu mbinu tunazotumia kwenye tovuti yetu.
Endelea Kugundua
Matokeo ni kwa madhumuni ya mifano na yanaweza kutofautiana. Unahitaji intaneti na usajili ili utumie vipengele fulani. Inapatikana kwa watumiaji wenye umri wa miaka 18 au zaidi. Tayarisha kwa kuwajibika.