Nufaika zaidi na Gemini
Pata usaidizi wa kila siku kutoka Google AI wa kushughulikia majukumu kazini, shuleni au nyumbani.
Ufikiaji wa 2.5 Flash
Ufikiaji unaodhibitiwa wa 2.5 Pro
Kubuni Picha ukitumia Imagen 4
Deep Research
Gemini Live
Canvas
Gem
Pata uwezo zaidi wa kutumia vipengele vipya na vyenye uwezo mkubwa ili uimarishe tija na ubunifu.
Pata ufikiaji wa kiwango cha juu zaidi wa vipengele bora zaidi vya Google AI pamoja na vipengele vya kipekee.
Gundua ubunifu wako ukitumia vipengele vyetu vinavyoongoza
Tayarisha kwa ufanisi zaidi
Ukiwa na ufikiaji zaidi wa mfumo wetu unaoongoza, 2.5 Pro, unaweza kubuni mikakati muhimu zaidi ya maudhui, kurahisisha taratibu zako za kazi, kubuni miundo mipya ya ubunifu na kugundua njia mpya za kuivutia hadhira yako ukitumia toleo jipya la mfumo unaoweza kushirikiana nao.
Panua wigo wako
Tekeleza miradi mikubwa kuliko hapo awali ukiwa na uwezo wa kupakia hadi kurasa 1,500 za faili. Tumia tafiti za sekta, manukuu ya video, rasilimali zako zilizopo na mengineyo ili utayarishe mawazo mapya ya maudhui yanayofaa mfumo wowote – kama vile machapisho ya kina kwenye blogu, manukuu ya mitandao ya kijamii na kurasa za tovuti.
Jifunze kwa haraka, elewa kwa kina na ujitayarishe kwa umahiri ili uwe miongoni mwa wanaoongoza.
Boresha uandishi wako
Usikwame tena unapotaka kuandika. Ikiendeshwa na mifumo yetu ya AI yenye uwezo zaidi, Gemini inaweza kukusaidia kupata rasimu ya kwanza, kuelezea hoja zako na kuboresha mawazo yako.
Kamilisha kazi yako ya shuleni ya kufanyia nyumbani
Pakia picha au faili ya kazi unayoifanya na Gemini itaichambua kwa kukupa mwongozo wazi wa hatua kwa hatua ili kukusaidia kuelewa jinsi ya kupata jibu.
Kamilisha hata miradi yako changamano zaidi, kwa haraka - iwe ni kujenga mawazo au kutekeleza
Boresha ujuzi
Andika hati, tayarisha nakala za mitandao ya kijamii na hata upate usaidizi wa kutambua washirika wa biashara ili uwe na muda zaidi wa kubuni.
Changanua maelezo mengi kama mtaalamu
Pakia hadi kurasa 1,500 za hati zako - iwe ni maoni ya wateja au mipango ya biashara na zaidi - ili upate usaidizi wa kitaalamu wa kuchanganua data yako, kupata maarifa muhimu na kutayarisha chati, hatua inayorahisisha jinsi unavyotekeleza miradi yako mahususi.
Boresha tija yako ya usimbaji
Tatua maswali changamano ukitumia msimbo wako
Pakia hazina yako ya misimbo, hadi mistari elfu 30 ya msimbo, ili Gemini ipitie mifano, ipendekeze maboresho muhimu, itatue matatizo ya vyanzo vya msimbo changamano, iboreshe mabadiliko mengi ya utendaji na itoe ufafanuzi kuhusu utaratibu wa sehemu mbalimbali za msimbo.
Boresha ujuzi wako wa usimbaji
Changia mawazo kuhusu suluhu, jadili mawazo ya miundo na upate majibu katika muda halisi kuhusu msimbo wako ili yakusaidie kuboresha ujuzi wako wa kutekeleza miradi binafsi au ustawi wa muda mrefu, yote kwa kutumia AI inayoshirikisha.
Pia, utaweza kutumia Gemini kwenye Chrome, Gmail, Hati na kupata manufaa mengine kutoka Google One
Whisk Animate
Dokeza ukitumia maneno na picha zako na uzigeuze ziwe klipu za sekunde 8 ukitumia mfumo wetu wa Veo 2, unaokuwezesha kutayarisha matukio yanayoweza kupanua mawazo na hadithi zako hata zaidi.
Gemini kwenye Gmail, Hati za Google na programu zaidi
Rahisisha majukumu yako ya kila siku na upate usaidizi wa kuandika, kupanga na kuonyesha data moja kwa moja katika programu za Google uzipendazo (inapatikana katika lugha mahususi).
Nafasi ya TB 2 kutoka Google One
Hifadhi nakala za faili na kumbukumbu zako kwa nafasi ya TB 2 ya kutumia katika Hifadhi ya Google, Gmail na huduma ya Picha kwenye Google. Pia, furahia manufaa zaidi kwenye bidhaa za Google.
NotebookLM
Pata vikomo vya juu vya matumizi na vipengele vya kulipiwa ukitumia NotebookLM ili vikusaidie kupata maarifa muhimu kwa haraka zaidi kutokana na maelezo unayoweka.
Project Mariner
Ukiwa na Project Mariner, unaweza kutumia mifumo tekelezi ya AI kurahisisha majukumu kama vile kupanga safari, kuagiza bidhaa na kuweka nafasi.
Gemini kwenye Gmail, Hati za Google na programu zaidi
Rahisisha majukumu yako ya kila siku na upate usaidizi wa kuandika, kupanga na kuonyesha data moja kwa moja katika programu za Google uzipendazo (inapatikana katika lugha mahususi).
Nafasi ya TB 30 kutoka Google One
Hifadhi nakala za faili na kumbukumbu zako kwenye nafasi ya TB 30 ya kutumia katika Hifadhi ya Google, Gmail na huduma ya Picha kwenye Google. Pia, furahia manufaa zaidi kwenye bidhaa za Google.
YouTube Premium
Furahia maudhui zaidi unayopenda, bila matangazo. Furahia YouTube na YouTube Music bila matangazo, nje ya mtandao na chinichini.
Anza jaribio lisilolipishwala Gemini AI Pro la mwezi moja
Maswali yanayoulizwa sana
Boresha hali yako ya kutumia programu ya Gemini kwa kujisajili kwenye mpango wa Pro. Tumia vipengele vipya na vyenye uwezo mkubwa ili utekeleze majukumu pamoja na miradi changamano.
Pata uwezo zaidi wa kutumia mifumo yetu bora, kama vile 2.5 Pro pamoja na vipengele vyenye uwezo mkubwa, ikijumuisha Deep Research na kiwango cha kubaini muktadha cha tokeni milioni 1. Pia, pata jaribio la muda mfupi la Veo 3 Fast, mfumo wetu wa kutayarisha video ulioboreshwa ili kuimarisha kasi na ufanisi.
Mpango wetu wa Google AI Pro unapatikana kwa watumiaji walio na umri wa zaidi ya miaka 18 na pia unajumuisha:
Gemini kwenye Gmail, Hati za Google na programu zaidi
Nafasi ya hifadhi ya TB 2
pamoja na manufaa mengine
Pia, unahitaji Akaunti binafsi ya Google unayoidhibiti mwenyewe.
Nufaika zaidi na Gemini kwa kujisajili kwenye mpango wa Ultra. Pata ufikiaji wa kiwango cha juu zaidi wa vipengele vyetu vyenye uwezo mkubwa kama vile utayarishaji wa video kwa kutumia Veo 3, Deep Research, mihtasari kwa sauti pamoja na mifumo yetu ya AI yenye uwezo zaidi kama vile 2.5 Pro Deep Think (itazinduliwa hivi karibuni). Pia, utapata kipaumbele cha kufikia ili ujaribu uvumbuzi wetu mpya zaidi wa AI kadiri unavyopatikana, ikiwa ni pamoja na Agent Mode.
Google AI Ultra inajumuisha kila kitu kwenye Google AI Pro na kwingineko. Google AI Ultra inapatikana kwa watumiaji walio na umri wa zaidi ya miaka 18 na pia inajumuisha:
Gemini kwenye Gmail, Hati za Google na programu zaidi
Nafasi ya TB 30
Whisk Animate
NotebookLM
pamoja na manufaa mengine
Pia, unahitaji Akaunti binafsi ya Google unayoidhibiti mwenyewe.
Ndiyo, hata hivyo, kunaweza kuwa na tofauti ya vipengele kati ya programu ya Gemini ya vifaa vya mkononi na programu ya Gemini ya wavuti. Jinsi ya kujisajili
Ikiwa ungependa kudhibiti usajili wako wa Google AI katika programu ya vifaa vya mkononi, gusa picha yako ya wasifu ili ufikie menyu ya Mipangilio.
Katisha usajili wa Google AI Pro wakati wowote kabla ya kipindi chako cha kujaribu kuisha. Hutarejeshewa pesa kwa vipindi vya bili visivyokamilika, isipokuwa kwa mujibu wa sheria inayotumika. Kwa kujisajili, unakubali sheria na masharti ya Google One, Google, na offers. Angalia jinsi Google inavyoshughulikia data. Google AI Pro na Gemini kwenye Gmail, Hati na programu zaidi zinapatikana tu kwa watumiaji walio na umri wa miaka 18 na zaidi. Gemini kwenye Gmail, Hati na programu zaidi inapatikana katika lugha mahususi. Vikomo vya matumizi vinaweza kutumika.