Nano Banana
Timiza ndoto zako.
Sasa unaweza kuchora mabadiliko yako kwenye Nano Banana. Hiki ni kiwango kipya kabisa cha udhibiti. Bofya kwenye picha yako, chora na ikiwa ungependa weka maandishi ili uweke maelezo mahususi. Gemini itashughulikia yaliyosalia.
Dial in every detail
with Nano Banana Pro.
Badilisha kabisa hali ya picha yako. Badilisha kutoka siku ya jua hadi usiku wa giza, cheza na pembe za kamera ili upate mwonekano bora na urekebishe umakinishaji ili mada yako iangaziwe.
Mtindo umetumika kwa sekunde chache.
Buni upya mwonekano wa picha yako. Chukua umbile, rangi au mtindo kutoka kwenye picha yoyote ya kurejelea na uitumie kwenye mada yako. Ni njia rahisi zaidi ya kujaribu miundo tofauti bila kuanzia mwanzo.
Picha moja, ukubwa mbalimbali.
Fanya kazi zako zionekane za kitaalamu popote unapozishiriki. Badilisha ukubwa wake papo hapo ili ulingane na muundo wowote unaohitaji – yote bila kupunguza vipengele unavyopenda.
Maneno yako, yamepangwa vizuri.
Buni nembo, mialiko, mabango, vibonzo na chochote unachohitaji ukitumia maandishi yaliyo wazi. Maneno yanafaa katika kazi yako, katika lugha nyingi.
Chagua mfumo unaofaa mahitaji yako
Chaguo bora kwa ubunifu wa haraka na wa kawaida.
Chaguo bora kwa matokeo ya kina na udhibiti mahususi.
Maswali yanayoulizwa sana
Kipengele cha kubuni picha kwa kutumia AI kinapatikana katika lugha zote na nchi zote ambamo programu ya Gemini inapatikana.
Ili ufikie Nano Banana, chagua ”🍌Buni picha” kwenye menyu ya zana na “Fast” kwenye menyu ya mifumo. Kisha uweke kidokezo au upakie picha ili uihariri.
Ili ufikie Nano Banana Pro, chagua ”🍌Buni picha” kwenye menyu ya zana na “Kutafakari” kwenye menyu ya mifumo. Kisha uweke kidokezo au upakie picha ili uihariri.
Kumbuka: Ukifikia kikomo chako cha kutumia Nano Banana Pro, utatumia kiotomatiki mfumo wa picha wa Nano Banana hadi ufikie kikomo hicho.
Anza na fomula rahisi. Jaribu <Tayarisha/buni picha ya> <mada> <kitendo> <tukio> kisha uendelee ukianzia hapo. Kwa mfano, "Tayarisha picha ya paka akiwa amelala chini ya mwale wa jua kwenye fremu ya chini ya dirisha."
Toa maelezo mahususi kadri ya ubunifu wako. Vidokezo vinapaswa kuwa na maelezo mengi mahususi kadri ya ubunifu wako, kwa hivyo, badala ya kusema, "Buni picha ya mwanamke aliyevaa nguo nyekundu," jaribu "Buni picha ya mwanamke aliyevaa nguo nyekundu huku akikimbia kwenye bustani." Kadri unavyotoa maelezo ya kina ndivyo Gemini itaweza kufuata maagizo yako.
Zingatia utunzi, muundo na ubora wa picha. Fikiria kuhusu jinsi unavyotaka vipengele vya picha yako vipangwe (utunzi), mwonekano unaoutaka (muundo), kiwango unachotaka cha ubora wa picha (ubora wa picha) na uwiano (ukubwa). Jaribu kitu kama vile, "Buni picha iliyotiwa ukungu ya nungu mwenye miba huku akipaa angani ukitumia mbinu ya upakaji rangi ya mafuta na uwiano wa 2:3."
Ubunifu wako utakusaidia. Gemini ni bora kwa kubuni vitu vya ajabu na matukio ya kipekee. Panua mawazo yako.
Usipopenda utakachoona, iombe Gemini ikibadilishe. Kupitia mfumo wetu wa kuhariri picha, unaweza kudhibiti picha zako kwa kuiambia Gemini ibadilishe mandharinyuma, ibadilishe kitu kimoja na kingine au iongeze kipengele huku ikihifadhi maelezo unayopenda.
Kulingana na Kanuni zetu za AI, Zana hii ya kubuni picha za AI iliundwa ili iweze kutumika kwa kuwajibika. Ili kuhakikisha kuwa kuna utofautishaji wazi kati ya picha zilizobuniwa na Gemini na kazi halisi ya sanaa ya binadamu, Gemini hutumia SynthID alama maalum isiyoonekana pamoja na alama maalum inayoonekana ili kuonyesha kuwa zimetayarishwa kwa AI.
Matokeo ya Gemini hutegemea kimsingi vidokezo vya mtumiaji na sawa na zana yoyote ya AI zalishi, kunaweza kuwa na matukio ambapo inatayarisha maudhui ambayo baadhi ya watu binafsi wanaweza kuyapinga. Tutaendelea kuzingatia maoni yako kupitia vitufe vya nimeipenda au sijaipenda na tutaendelea kufanya maboresho. Kwa maelezo zaidi, unaweza kusoma kuhusu mbinu tunazotumia kwenye tovuti yetu.
Pakia tu picha kwenye programu ya Gemini kisha uulize iwapo ilitayarishwa na Google AI. Uthibitishaji huu unawezeshwa na SynthID, teknolojia yetu ya kuweka alama maalum dijitali. Kwa sasa inapatikana kwa picha, usaidizi wa sauti na video utapatikana hivi karibuni.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoongeza uwazi katika maudhui ya AI kwa kutumia SynthID kwenye chapisho letu la blogu.
Uoanifu na upatikanaji hutofautiana. Vikomo vinatumika. 18+.