Skip to main content

Gemini Deep Research

Okoa muda ukitumia Deep Research kama msaidizi wako binafsi wa utafiti
Inaendeshwa na Gemini 2.0 Flash Thinking (jaribio), sasa ina Muhtasari kwa Sauti

Deep Research ni nini?

Pata maelezo haraka kuhusu kitu chochote ukitumia Deep Research, kipengele cha kutekeleza majukumu changamano kwenye Gemini, kinachoweza kuvinjari hadi mamia ya tovuti kiotomatiki kwa niaba yako, kuchanganua matokeo kinayopata na kutayarisha ripoti zilizo na maarifa ya kina zenye kurasa nyingi unazoweza kubadilisha ziwe mazungumzo yanayoshirikisha yanayofanana na podikasti.

Kupanga

Deep Research hubadilisha kidokezo chako kuwa mpango wa utafiti uliowekewa mapendeleo wenye sehemu nyingi

Kutafuta

Deep Research hutafuta kwa njia huru na kuvinjari wavuti kwa kina ili kutafuta maelezo muhimu na ya hivi punde

Kuchanganua dhana

Deep Research huonyesha mawazo yake inapochanganua maelezo iliyokusanya kwa njia endelevu na kufikiri kabla ya kuchukua hatua inayofuata

Kuripoti

Deep Research hutoa ripoti maalum za kina za utafiti zenye maarifa na maelezo zaidi. Ripoti hutayarishwa ndani ya dakika chache na zinapatikana kama Muhtasari kwa Sauti, hali inayokusaidia kuokoa muda

Jinsi ya kutumia Deep Research

Gemini Deep Research imeundwa ili kutekeleza majukumu ya utafiti changamano kwa kuyachambua, kutafuta majibu kwenye wavuti na kutayarisha matokeo ya kina.

Kwa kutumia 2.0 Flash Thinking (jaribio), Gemini imeboreshwa zaidi katika hatua zote za utafiti, iwe ni kupanga au kutayarisha ripoti zenye maelezo na maarifa ya kina. Sasa, unaweza pia kubadilisha ripoti yako kuwa Muhtasari kwa Sauti ili uendelee kupata taarifa hata wakati unatekeleza majukumu mengi.

Uchanganuzi wa ushindani

Kuelewa mazingira ya washindani wa bidhaa mpya, ikiwa ni pamoja na ofa, bei, utangazaji na maoni ya wateja.

Uhakiki

Kuchunguza wateja watarajiwa wanaoweza kununua, kuchambua bidhaa za kampuni, historia ya ufadhili, timu na mazingira ya ushindani.

Kuelewa mada

Kuchanganua mada kwa kina kwa kulinganisha na kutofautisha dhana muhimu, kubaini uhusiano kati ya mawazo na kuelezea kanuni zinazohusiana nayo.

Kulinganisha bidhaa

Kutathmini mifumo tofauti ya bidhaa kulingana na vipengele, utendaji, bei na maoni ya wateja.

Ni hatua ya kufikia AI saidizi inayoweza kuwa mshirika wa kushirikiana naye mwenye uwezo zaidi wa kutekeleza na kuchanganua dhana badala ya kujibu tu maswali unayoiuliza.

Ijaribu leo bila kulipia.

Anza kuitumia

Msimamizi Mkuu wa Deep Research, Aarush Selvan, anaelezea kuhusu kutumia Deep Research kwa mara ya kwanza.

Jinsi ya kufikia Deep Research

Jaribu Deep Research leo bila kulipia

  • Katika kompyuta ya mezani

  • Kwenye simu

  • Katika nchi 150

  • Katika zaidi ya lugha 45

  • Na kwa watumiaji wa Google Workspace

Chagua tu Deep Research kwenye menyu kunjuzi ya kuteua mfumo au upau wa kidokezo ili uanze kutumia na uiruhusu Gemini ikufanyie utafiti.

Watumiaji wa Gemini Advanced wana ufikiaji uliopanuliwa wa Deep Research.

Jinsi tulivyobuni toleo la kwanza la Deep Research

Siku ya kwanza baada ya kuanzisha Deep Research kwenye Gemini mnamo Desemba 2024, tulikusanya baadhi ya washiriki wa timu inayoishughulikia ili kufanya majadiliano.

Mfumo wenye uwezo wa kutekeleza majukumu

Ili kubuni Deep Research, tulianzisha mfumo mpya wa kupanga unaowezesha programu ya Gemini kutekeleza majukumu changamano. Kwa Deep Research, tuliifundisha mifumo ya Gemini iweze:

  • Kuchanganua suala: Ikipatiwa hoja changamano ya mtumiaji, mfumo kwanza unatayarisha mpango wa kina wa utafiti, ukichanganua suala katika masuala madogo yanayoweza kutekelezwa kwa urahisi. Unadhibiti mpango: Gemini inakupatia mpango na unaweza kuuboresha ili kuhakikisha kuwa unaangazia sehemu zinazofaa.

  • Kutafiti: Mfumo huu unasimamia utekelezaji wa mpango huu na kubaini kwa umahiri majukumu madogo yanayowezwa kutekelezwa kwa wakati mmoja na yale yanayohitaji kutekelezwa kwa mfululizo. Mfumo unaweza kutumia zana kama vile utafutaji na kuvinjari kutafuta maelezo na kuyachanganua. Katika kila hatua, mfumo huchanganua maelezo yanayopatikana ili kuamua hatua utakaochukua. Tulizindua kidirisha cha kuchanganua dhana ili watumiaji wafuatilie kile ambacho mfumo umejifunza utafiti unapoendelea na unachokusudia kufanya baadaye.

  • Kusanisi: Baada ya mfumo kubaini kuwa maelezo ya kutosha yamekusanywa, unasanisi matokeo kuwa ripoti ya kina. Katika kutayarisha ripoti, Gemini hutathmini maelezo kwa kina, hubainisha mada muhimu na utofauti na kutayarisha ripoti hiyo kwa njia ya kimantiki na ya kuelimisha, hata kwa kutekeleza mbinu nyingi za kujihakiki ili kuboresha ubayana na maelezo.

Aina mpya, matatizo mapya, suluhu mpya

Wakati tunabuni Deep Research, ilitupasa kushughulikia changamoto tatu kubwa za kiufundi:

Kupanga kwa hatua nyingi

Majukumu ya utafiti yanahitaji hatua nyingi za kupanga kwa kutumia uboreshaji endelevu wa haraka. Katika kila hatua, mfumo unapaswa kujiyakini kuhusu maelezo yote yaliyokusanywa kwa wakati huo, kisha utambue maelezo yanayokosekana na tofauti unazotaka kugundua — huku ukilinganisha ukamilifu na muda wa mtumiaji kusubiri na wa kutekeleza. Kufundisha mfumo ufae katika kupanga hatua nyingi ndefu kwa namna yenye ufanisi wa data kulituwezesha kufanya Deep Research itekeleze majukumu katika mipangilio ya mfumo unaoweza kushughulikia mada zote.

Makisio ya muda mrefu

Jukumu la kawaida la Deep Research linajumuisha mifumo mingi kutekeleza ndani ya dakika kadhaa. Hali hii inasababisha changamoto katika kubuni visaidizi: Inapaswa kutengenezwa ili hitilafu moja isisababishe jukumu litekelezwe upya kuanzia mwanzo.

Ili kushughulikia hili, tulisanidi kidhibiti kipya cha shughuli kisichosawazisha ambacho kinadumisha hali ya pamoja kati ya kiratibu na mifumo ya majukumu, hali inayoruhusu usuluhishaji mzuri wa hitilafu bila kutekeleza upya jukumu lote. Mfumo huu hausawazishi: unaweza kwenda kwenye programu tofauti au kuzima kompyuta yako baada ya kuanzisha mradi wa Deep Research na ukitembelea Gemini wakati ujao, utaarifiwa utafiti wako utakapokamilika.

Kudhibiti muktadha

Katika kipindi cha utafiti, Gemini inaweza kuchakata mamia ya kurasa za maudhui. Ili kudumisha mwendelezo na kuruhusu maswali ya nyongeza, tunatumia kiwango cha Gemini cha kubaini muktadha cha tokeni milioni 1 kinachoongoza katika sekta pamoja na mipangilio ya RAG. Kwa ufanisi, hatua hii inauwezesha mfumo "ukumbuke" kila kitu ulichojifunza katika kipindi hicho cha gumzo, hali inayoufanya uwe mahiri zaidi kadiri unavyoutumia.

Sasa inaendeshwa na 2.0 Flash Thinking (jaribio)

Deep Research ilipozinduliwa mnamo Desemba, ilikuwa inaendeshwa na Gemini 1.5 Pro. Kwa kuzindua Gemini 2.0 Flash Thinking (jaribio), tuliweza kuimarisha kwa kiwango kikubwa ubora na ufanisi wa huduma hii katika kutekeleza majukumu. Kwa mifumo ya kuchanganua dhana, Gemini inachukua muda zaidi kupanga mbinu itakazotumia kabla ya kuchukua hatua. Sifa hii halisi ya kujitathmini na kupanga inaifanya ifae zaidi aina hizi za majukumu changamano ya muda mrefu. Tunachoona ni kuwa kwa sasa Gemini ni bora zaidi katika hatua zote za utafiti na inatayarisha ripoti za kina. Kwa wakati huo huo, ufanisi wa kutekeleza majukumu wa mfumo wa Flash unatuwezesha kupanua ufikiaji wa Deep Research kwa watumiaji zaidi. Kwa ujumla, tuna furaha sana kuhusu kubuni mifumo ya Flash na Thinking na tunatarajia kuendelea kuboresha Deep Research.

Kinachofuata

Tulibuni mfumo uwe thabiti, kwa hivyo kadiri muda unavyosonga, tunaweza kuongeza uwezo wake kwa kukupatia udhibiti zaidi wa kile unachoweza kuvinjari na kutoa vyanzo vyake kando na wavuti huria.

Tunafurahia kuona jinsi watu wanavyotumia Deep Research na hali hizi halisi zitachangia jinsi tunavyoendelea kubuni na kuboresha Deep Research. Mwishowe, lengo letu ni kubuni kiratibu muhimu kinachotumia AI cha kutekeleza majukumu mengi na changamano.

Gemini ya Kutekeleza Majukumu Changamano

Changanua dhana
Tafuta
Vinjari

Mfumo mpya wa AI saidizi wa Gemini huleta pamoja ubora wa Gemini, huduma ya Tafuta na Google pamoja na teknolojia za wavuti ili kuendelea kutafuta, kuvinjari na kuchanganua maelezo katika hali ya kurudia hoja ili kupata matokeo ya kina zaidi.