Skip to main content
Gemini Advanced

Furahia mifumo ya AI ya Google yenye uwezo zaidi, kipaumbele cha kutumia vipengele vipya na kiwango cha kubaini muktadha cha tokeni milioni 1

Gemini

Kiratibu chako cha binafsi kinachotumia AI kutoka Google. Piga gumzo na Gemini
ili uchochee zaidi mawazo yako

$0 USD kwa mwezi
  • Tumia mfumo wetu wa Gemini 1.5 Flash

  • Kiwango cha kubaini muktadha cha tokeni elfu 32 kwa mazungumzo marefu ya kujibizana

  • Pata usaidizi wa kuandika, kupanga, kujifunza, kubuni picha na shughuli nyingine

  • Kusanya maelezo na utekeleze mambo katika programu mbalimbali za Google kwa wakati mmoja

Gemini Advanced

Idhini yako ya kutumia toleo jipya la AI kutoka Google bila mipaka. Inajumuisha kila kitu kwenye Gemini na kwingineko.

$ 19.99 USD kwa mwezi
$0 USD kwa mwezi wa kwanza
  • Tumia toleo jipya la mfumo wetu, 1.5 Pro

  • Kiwango cha kubaini muktadha cha tokeni milioni 1, kikiwa na uwezo wa kushughulikia upakiaji wa hadi kurasa 1,500

  • Kipaumbele cha kutumia vipengele vipya zaidi vya Gemini

  • Nafasi ya hifadhi ya TB 2 kutoka Google One*

  • Gemini katika Gmail, Hati na viendelezi zaidi (inapatikana katika lugha mahususi)*

*Inajumuishwa na usajili wako kama sehemu ya mpango wako wa Google One Ya Juu yenye AI

Pata kipaumbele cha kutumia vipengele vipya zaidi vya Gemini

Ukiwa na Gemini Advanced, utaweza kushughulikia miradi yako changamano zaidi na kupata kipaumbele cha kutumia vipengele vipya zaidi vya AI kutoka Google pindi vinapopatikana.

Tayarisha ripoti za kina zenye kurasa nyingi kwa haraka

Pata maelezo haraka kuhusu mada yoyote unapotumia Deep Research. Hubadilisha kidokezo chako kuwa mpango wa utafiti wenye sehemu nyingi, inaweza kuvinjari kiotomatiki mamia ya tovuti ili kutafuta maelezo ya hivi punde na hutayarisha ripoti za kina zenye maarifa yanayofaa zaidi—yote ndani ya muda mfupi.2

Inapatikana kwa sasa katika Kiingereza pekee.

Ruhusu maelezo kuhusu mapendeleo yako yafikiwe ili upige gumzo kwa ufanisi zaidi

Iombe Gemini ikumbuke mapendeleo yako na mambo yanayokuvutia, yakiwemo kazi, mambo uyapendayo na malengo, ili ikupatie majibu bora yanayofaa. Unaweza kuangalia, kubadilisha au kufuta maelezo yoyote unaliyoruhusu yafikiwe, kwa urahisi na uone pale yanapotumiwa.

Inapatikana kwa sasa katika Kiingereza pekee.

Rahisisha majukumu ukitumia matoleo maalum ya Gemini

Tumia Gem kubuni viratibu maalum vya AI vilivyo na utaalamu wa mada yoyote. Gem inaweza kuwa chochote kama vile mkufunzi wa taaluma, kihariri cha wasifukazi au hata kisaidizi cha usimbaji. Tumia mkusanyiko wetu wa Gem zilizobuniwa mapema au ubuni yako mwenyewe ili ikusaidie kutimiza malengo yako na kukamilisha majukumu kwa haraka.3

Majukumu changamano yanahitaji AI iliyoboreshwa

Iwe unatuma ombi ya kujiunga na chuo, unabadilisha taaluma, unaanza kutekeleza mawazo ya ubunifu au unafungua shughuli ya kukuingizia kipato cha ziada, kuna wakati utahitaji usaidizi zaidi.

upload icon

Nisaidie kujifunza

Pakia madokezo ya darasani na Gemini Advanced inaweza kuandaa mihtasari ya dhana muhimu, kutayarisha mitihani ya majaribio na kukupatia maelezo ili uelewe vyema nyenzo za kozi

search icon

Nisaidie kuchanganua

Safisha na uchanganue data kutoka kwenye malahajedwali yako ili ugundue maarifa kwa haraka na utayarishe chati zilizo tayari kuwasilishwa

lightbulb icon

Nisaidie kubuni

Harakisha mchakato wako wa ubunifu kwa kushirikiana na Gemini Advanced ili uchochee mawazo mapya, ujadili kuhusu miradi na upate usaidizi kwenye rasimu zako za kwanza

code icon

Nisaidie kusimba

Pata usaidizi wa ziada wa kujifunza dhana mpya za usanidi na uokoe muda katika kutayarisha, kuhariri na kukagua msimbo wako

Pia, utaweza kutumia Gemini katika Gmail, Hati na viendelezi zaidi, kupata nafasi ya hifadhi ya TB 2 na manufaa mengine kutoka Google One

Gmail and Docs icons

Gemini katika Gmail, Hati na viendelezi zaidi (inapatikana katika lugha mahususi)

Google One icon

Nafasi ya hifadhi ya TB 2 na manufaa mengine ya Google One

Anza kipindi cha kujaribu bila kulipishwa cha mwezi 1

Maswali yanayoulizwa sana

Shughulikia miradi yako changamano zaidi ukitumia Gemini Advanced, idhini yako ya kutumia toleo jipya la AI kutoka Google bila mipaka. Furahia mifumo yetu ya AI yenye uwezo zaidi, kipaumbele cha kutumia vipengele vipya na kiwango cha kubaini muktadha cha tokeni milioni 1.

Gemini Advanced iliyo na mifumo yetu ya AI yenye uwezo zaidi inapatikana tu kwa watumiaji walio na umri wa zaidi ya miaka 18 kama sehemu ya mpango wa Google One Ya Juu yenye AI ambao pia unajumuisha:

  • Gemini katika Gmail, Hati na viendelezi zaidi

  • Nafasi ya hifadhi ya TB 2

  • pamoja na manufaa mengine

Pia, unahitaji Akaunti ya Google ya binafsi unayoidhibiti mwenyewe. Jinsi ya kujisajili

Gemini Advanced iliyo na mifumo yetu ya AI yenye uwezo zaidi inapatikana tu kwa watumiaji walio na umri wa zaidi ya miaka 18 kama sehemu ya mpango mpya wa Google One Ya Juu yenye AI ambao pia unajumuisha:

  • Gemini katika Gmail, Hati na viendelezi zaidi

  • Nafasi ya hifadhi ya TB 2

  • pamoja na manufaa mengine

Pia, unahitaji Akaunti ya Google ya binafsi unayoidhibiti mwenyewe.

Iwapo unatimiza masharti, unaweza kujisajili uanze kutumia Gemini Advanced sasa hivi. Pia, unaweza kujisajili moja kwa moja katika Programu za Gemini: Unapaswa kuona kitufe cha kujisajili kwenye menyu.

Ndiyo, hata hivyo, kunaweza kuwa na tofauti ya vipengele kati ya programu ya Gemini ya vifaa vya mkononi na programu ya Gemini ya wavuti. Jinsi ya kujisajili

Ikiwa ungependa kudhibiti usajili wako wa Gemini Advanced katika programu ya vifaa vya mkononi, gusa picha yako ya wasifu ili ufikie menyu ya Mipangilio.

Tunaamini katika kutumia mfumo unaofaa kwenye jukumu linalofaa. Tunatumia mifumo mbalimbali tuliyo nayo kwenye majukumu mahususi kulingana na tunachofikiria kwamba kitakupatia hali bora zaidi ya utumiaji.

Ukitumia Gemini Advanced, unaweza kufikia mifumo yetu ya AI iliyo na uwezo zaidi.

Katisha usajili wa Google One Ya Juu yenye AI wakati wowote kabla ya kipindi chako cha kujaribu kuisha. Hutarejeshewa pesa kwa vipindi vya bili visivyokamilika, isipokuwa kwa mujibu wa sheria inayotumika. Kwa kujisajili, unakubali sheria na masharti ya Google OneGoogle, na ofa. Angalia jinsi Google inavyoshughulikia data. Gemini Advanced na Gemini ya kutumia kwenye Gmail, Hati na viendelezi zaidi zinapatikana tu kwa watumiaji walio na umri wa miaka 18 na zaidi. Gemini ya kutumia kwenye Gmail, Hati na viendelezi zaidi inapatikana katika lugha mahususiVikomo vya matumizi vinaweza kutumika.