Hujambo, Gemini
Tunakuletea kiratibu cha kila siku kinachotumia AI kutoka Google
Uliza maswali changamano
Ungependa kuelewa mchakato wa kurudufisha DNA au jinsi ya kutengeneza kitu ukitumia mkono? Gemini imeyakinishwa kwenye huduma ya Tafuta na Google hivyo unaweza kuiuliza kuhusu kitu chochote na kuuliza maswali ya nyongeza hadi upate kuelewa vyema.
Buni picha kwa haraka
Ukitumia Imagen 3, mfumo wetu mpya kabisa wa kubuni picha, unaweza kupata hamasa ya muundo wa nembo, kugundua miundo mbalimbali iwe ni vibonzo au michoro ya mafuta na kubuni picha kwa kuandika vidokezo vya maneno machache. Ukishabuni, unaweza kuwatumia wengine au kupakua papo hapo.
Zungumza na Gemini Live
Fanya majadiliano ya mawazo kwa sauti, fanya mazoezi ya kujibu maswali ya mahojiano, tuma faili au picha ambayo ungependa kujadili kuihusu na ujadili na Gemini Live.
Tumia muda mfupi kuandika
Kamilisha mambo kwa haraka. Tumia Gemini kuandaa muhtasari wa maandishi, kutayarisha rasimu za kwanza na kupakia faili ili upate maoni kuhusu vitu ambavyo tayari umeandika.
Boresha masomo yako
Buni mipango ya masomo, mihtasari ya mada na maswali ili ujaribu maarifa yako. Unaweza hata kufanya mazoezi ya mawasilisho na Gemini Live kwa sauti.
Pata usaidizi wa kutekeleza majukumu katika programu mbalimbali kwa wakati mmoja
Gemini huunganisha na vitu vyako kwenye Gmail, Kalenda ya Google, Ramani za Google, YouTube na huduma ya Picha kwenye Google ili kukusaidia kupata unachotaka bila kubadilisha kati ya programu. Unaweza kutumia Gemini kuweka kengele, kudhibiti muziki na kupiga simu bila kugusa kifaa.
Fupisha muda wa kutafuta ukitumia Deep Research
Pitia mamia ya tovuti, changanua maelezo na utayarishe ripoti ya kina kwa haraka. Ni sawa na kuwa na mhudumu wa utafiti anayekufaa ambaye anakusaidia kutekeleza kwa haraka jukumu lolote.
Buni viratibu maalum ukitumia Gem
Hifadhi maagizo ya kina zaidi na upakie faili ili ukipatie muhtasari kiratibu chako kinachotumia AI. Gem inaweza kuwa chochote kama vile mkufunzi wa taaluma, mshirika wa kuchangia mawazo au hata kisaidizi cha usimbaji.
Kagua hazina kubwa za misimbo na faili
Kwa kutumia kiwango kikubwa cha kubaini muktadha cha tokeni milioni 1, Gemini Advanced inaweza kuelewa na kuchanganua vitabu kamili, ripoti ndefu na mengineyo kwa kupakia hadi kurasa 1,500 au mistari elfu 30 ya misimbo, yote kwa wakati mmoja.
Mipango
Kiratibu chako cha binafsi kinachotumia AI kutoka Google. Piga gumzo na Gemini ili uboreshe mawazo yako.
-
Uwezo wa kufikia mfumo wa 2.0 Flash na mifumo yetu ya majaribio ikiwa ni pamoja na 2.5 Pro
-
Zungumza kwa urahisi na Gemini Live, popote ulipo
-
Tayarisha ripoti za kina ukiwa na ufikiaji unaodhibitiwa wa Deep Research
-
Tumia Gem kubuni na kutumia viratibu maalum vya AI vilivyo na utaalamu wa mada yoyote
-
Pata usaidizi wa kutekeleza majukumu katika programu mbalimbali za Google kwa wakati mmoja
Idhini yako ya kutumia toleo jipya la AI kutoka Google bila mipaka. Inajumuisha kila kitu kwenye Gemini na kwingineko.
-
Ufikiaji uliopanuliwa wa mfumo wetu wa majaribio wa hali ya juu, 2.5 Pro
-
Elewa ripoti na vitabu vikubwa vilivyo na kurasa 1,500 za faili zilizopakiwa
-
Pata ufikiaji uliopanuliwa wa Deep Research ili uokoe muda zaidi kwenye miradi changamano
-
Andika misimbo kwa umahiri na kwa haraka kwa kupakia hazina yako ya misimbo
-
Ina TB 2 za nafasi ya hifadhi kutoka Google One*
-
Rahisisha majukumu yako ukiwa na ufikiaji wa Gemini kwenye Gmail, Hati na programu nyingine* (inapatikana katika lugha mahususi)
-
NotebookLM Plus yenye kima cha mara 5 zaidi cha matumizi na vipengele vya kulipiwa*
*Inajumuishwa na usajili wako kama sehemu ya mpango wa Google One Ya Juu yenye AI
Je, wewe ni mwanafunzi?
Angalia iwapo unatimiza masharti yetu ya punguzo la wanafunzi.