Wanafunzi: pata idhini ya kutumia Omni bila kulipia kwa mwaka mmoja. Muda wa ofa utaisha hivi karibuni. Learn more
Skip to main content

Gemini Omni
Zungumza. Angalia. Tuma.

Gemini Omni hurahisisha utayarishaji wa video kupitia mazungumzo. Ichukulie kama Nano Banana ya video. Anzia mwanzo, badilisha matunzio yako upendavyo au ujaribu kiolezo kilichobuniwa mapema.

Bado hujaanza kutumia kifurushi kinacholipiwa? Pandisha daraja ili upate idhini ya kutumia Gemini Omni na zaidi.

Tayarisha klipu kutokana na dhana.

Gemini Omni ni mfumo wako wa ubunifu wa kutayarisha maudhui ya miundo anuai.

Mpya

Anza kutayarisha maudhui.

Weka avata yako ya AI mara moja tu ili utayarishe maudhui yasiyo na kikomo yanayofanana na kusikika kama wewe.

Mpya

Refusha tukio.

Iulize Gemini kuhusu kitakachofuata ili urefushe video yako huku ukidumisha simulizi.

Keep the soul of the shot.

Badilisha mandharinyuma, mavazi au uhamishe mitindo huku ukihifadhi maelezo yako.

Instant inspiration.

Usisubiri wazo. Anza kutumia mitindo iliyoratibiwa ili uone unachoweza kufanikisha kwa kugusa mara moja.

Easy editing.

Iambie tu Gemini kitu cha kurekebisha. Badilisha wahusika, rekebisha mwangaza, imarisha video au ubadilishe mandharinyuma ukitumia gumzo.

Washirikishe marafiki zako kwa kutuma avata.

Tuma simulizi hii kwa marafiki zako kwa kubadilishana avata zenu maalum kwa njia salama ili msimuliane hadithi, mchangie mawazo na kuwashirikisha katika ulimwengu wako wa ubunifu.

Buni

Tayarisha video na uhuishaji wenye ubora wa juu unaokupa uhuru wa kujieleza kwa namna ambayo hujawahi kuipata awali.

Tuma

Badilishana idhini ya kutumia avata na marafiki zako ili mpeane nafasi kuu za uhusika katika chochote mnachobuni kwa pamoja

Dhibiti

Decide who can create with your avatar and when they are allowed to use it.

Buni chochote. Kutokana na kila kitu.

Changanya maandishi, picha na video ili utekeleze mawazo yako kuwa uhalisia unaojongea.

Karibu kwenye Gemini Omni.

Tunaendelea kuboresha mifumo yetu na kutafuta njia za kurahisisha zaidi mchakato wako wa ubunifu. Gemini Omni itachukua nafasi ya Veo kwenye programu ya Gemini. Omni inajumuisha umaizi wa msingi wa Gemini na uwezo wa hali ya juu wa mifumo ya kutayarisha maudhui ikiwa ni pamoja na kubadilisha picha kuwa video na kuhariri video kwa kutumia AI. Inaelewa ulimwengu, huchanganya aina tofauti za maudhui na hukupa udhibiti zaidi wa kuhariri. Tumia Omni kwa mahitaji yako yote ya kuhariri na kutayarisha video kwa kutumia AI.

Gemini Omni 1.1 Flash

Mfumo wa AI wa kutayarisha video na kuhariri maudhui ya miundo anuai ambao sasa utachukua nafasi ya mfumo wa awali wa Google Gemini Veo 3.1.

Checkmark
Tayarisha video za sekunde 10
Checkmark
Mfumo kutayarisha sauti
Checkmark
Tayarisha video kutokana na picha (hadi 5)
Mpya
Viendelezi vya matukio
Mpya
Kuhariri video kuwa video nyingine
Mpya
Kuhariri kwa hatua nyingi
Mpya
Avata

Unahitaji kuwa na usajili wa Google AI. Vipengele hutofautiana kulingana na kiwango na maeneo ya kijiografia. 18+.

Maswali yanayoulizwa sana

Gemini Omni Flash ni mfumo unaoelewa mazingira yako ili uweze kuhuisha picha au kutayarisha video kutokana na maudhui yoyote. Ikitokana na uwezo wa Gemini wa kuelewa mazingira ya uchakataji na utojai asili wa maudhui ya miundo anuai, Gemini Omni hutayarisha matokeo yanayoonyesha mantiki ya ulimwengu halisi na hukuwezesha kuyabuni hatua kwa hatua kupitia mazungumzo ya kawaida. Unaweza kuwa mhariri wa video anayetumia AI kwa kutumia kidokezo tu.

Unachoweza kufanya ukitumia Gemini Omni:

  • Badilisha mchanganyiko wowote wa maandishi, picha au video kuwa video

  • Tayarisha video kutokana na marejeleo ya picha (hadi 5)

  • Hariri video kwa urahisi

  • Refusha matukio ili simulizi liendelee

Tunatafuta kila wakati njia za kufanya zana zetu za AI ziwe na manufaa na ubunifu zaidi kwa watumiaji. Gemini Omni ni mfumo wetu mpya kabisa wa kuhariri na kutayarisha video ambao utachukua nafasi ya Veo katika programu ya Gemini.

We’ve seen how creators have been making videos from photos and adding themselves into their creations. Now, we’re making that process even easier with AI avatars. An avatar is a digital version of yourself that lets you generate videos that look and sound like you, safely and securely.

Zaidi ya yote, matumizi ya kipengele hiki ni ya hiari kabisa na ni wewe pekee unaweza kutumia avata yako kutayarisha video. Unaweza kuendelea kupakia picha zako au uruke hatua ya ziada na utumie avata yako. Pata maelezo zaidi kuhusu avata za AI hapa.

Kulingana na kanuni zetu za AI, video zote zinazotayarishwa kwenye programu ya Gemini hupachikwa SynthID, alama yetu maalum isiyoonekana ya kutambua maudhui yaliyotayarishwa kwa Google AI.

Pia tunakupa njia zaidi za kusaidia kutambua maudhui ya AI, tukipanua uwezo wetu wa uthibitishaji ili kujumuisha picha, video na sauti. Pakia tu faili kisha uulize iwapo imetayarishwa kwa kutumia Google AI na Gemini itakagua SynthID na kutumia uwezo wake wa kuchanganua ili kutoa jibu.