Skip to main content

Tunakuletea Gemini kwenye Chrome

Usaidizi wa AI, moja kwa moja katika kivinjari chako.

Akiliunde inayokusaidia, popote ulipo.

Pata hoja muhimu, fafanua dhana na upate majibu kulingana na muktadha wa vichupo ulivyofungua.

Ungependa kuelewa hoja muhimu kwa haraka? Gemini huandaa mihtasari mifupi ya makala, kurasa au mazungumzo moja kwa moja katika kivinjari chako, ili uelewe hoja kuu kwa haraka.

Una swali kuhusu kitu unachosoma? Uliza Gemini. Gemini hutumia muktadha wa vichupo ulivyofungua kutoa ufafanuzi na majibu yanayofaa, ili uendelee kumakinika.

Fahamu mambo mengine kando na ufafanuzi rahisi. Unaposhughulikia mada changamano au dhana mpya, iombe Gemini ikusaidie kujishirikisha na maudhui husika kando na kufafanua sehemu tatanishi tu.

Je, unatafiti kuhusu bidhaa au kulinganisha chaguo? Iombe Gemini ikupe maelezo muhimu, sifa mahususi au manufaa na upungufu kutoka kwenye ukurasa, ili kukusaidia kufanya uamuzi bora kwa ubayana na urahisi.

Ungependa kujadili mawazo, kupanga hoja au kugundua zaidi kuhusu mada fulani? Piga gumzo na Gemini Live kwa njia ya kawaida na upate majibu yanayotamkwa, yote katika Chrome.

Kama ilivyo kwenye kompyuta yako, Gemini katika simu inaweza kujibu maswali kuhusu kitu unachosoma. Kwenye Android, Gemini hufanya kazi na chochote kilicho katika skrini yako—ikiwa ni pamoja na Chrome. Hivi karibuni, Gemini itajumuishwa kwenye programu ya Chrome katika iOS.

Unadhibiti matumizi yako ya wavuti

Gemini kwenye Chrome hukusaidia katika kazi zako, kulingana na masharti yako. Inakusaidia tu unapoiomba, kwa hivyo una udhibiti.

Huwa tayari ukiwa tayari

Gemini kwenye Chrome huwashwa tu unapochagua kuitumia kwa kubofya aikoni ya Gemini au mikato ya kibodi uliyoweka. Inakusaidia unapoiomba, kulingana na masharti yako.

Pata usaidizi, unapouhitaji

Pata usaidizi unapouhitaji ukitumia Gemini kwenye Chrome. Zungumza au uandike swali lako kwa njia ya kawaida na Gemini inaweza kutumia maudhui ya ukurasa kukusaidia kuyaelewa kwa haraka au kukamilisha majukumu yanayochosha.

Dhibiti shughuli zako kwa urahisi

Unaweza kufikia Shughuli zako kwenye Programu za Gemini wakati wowote ili udhibiti, ufute na uzime shughuli zako.

Wavuti umebuniwa upya.

Ukitumia Gemini kwenye Chrome, hutahitaji kubadilisha vichupo ukipata usaidizi wa AI moja kwa moja katika kivinjari chako, unaokusaidia kuelewa maudhui kwa haraka au kukamilisha majukumu kwa kutumia muktadha wa vichupo ulivyofungua.

Maswali yanayoulizwa sana

Ukitumia kipengele cha Gemini kwenye Chrome, unaweza kupata usaidizi wa AI katika kivinjari chako ili ufanye mambo kwa urahisi kama vile kupata hoja muhimu, kufafanua dhana, kupata majibu na mengine mengi. Ili kukupa majibu yanayokufaa zaidi, Gemini kwenye Chrome hutumia muktadha wa vichupo ulivyofungua. 

Gemini kwenye Chrome ni sehemu ya kivinjari cha Chrome katika kompyuta za mezani na ni tofauti na kutumia Gemini kwenye kivinjari chochote katika gemini.google.com au kuanzisha gumzo na programu ya Gemini ya wavuti kwa kuandika @gemini katika sehemu ya anwani kwenye Chrome. Unaweza kutumia programu ya Gemini ya wavuti katika vivinjari vingine (au sehemu ya maudhui ya Chrome), lakini hutaweza kutuma maudhui ya ukurasa au kutumia hali ya Live kama unavyoweza kufanya ukitumia Gemini kwenye Chrome.

Unaweza kufikia Gemini kwenye Chrome kupitia aikoni ya Gemini katika upau wa vidhibiti wa Chrome au kupitia mikato ya kibodi unayoweka kwenye kompyuta ya mezani ya Windows au Mac.

Pia unaweza kuwasha Gemini unapotumia Chrome kwenye Android na programu nyingine kwa kushikilia kitufe cha kuwasha au kuzima. Na hivi karibuni, Gemini kwenye Chrome itajumuishwa katika programu kwenye iOS na utaweza kuifikia kupitia sanduku kuu la Chrome.

Gemini kwenye Chrome inasambazwa kwa watumiaji wote wa Mac na Windows wanaotimiza masharti walioko Marekani ambao wanatumia Chrome katika Kiingereza. Tunatazamia kusambaza kipengele hiki kwa watu wengi na katika lugha zaidi hivi karibuni.

Hivi karibuni, Gemini kwenye Chrome itapatikana katika iOS kwa watumiaji wa iPhone wanaotimiza masharti walioko Marekani ambao wanatumia Chrome katika Kiingereza.

Kagua majibu. Unahitaji kuweka mipangilio. Uoanifu na upatikanaji hutofautiana. 18+